Iramba in Dar es Salaam Development Club
(IDA) ni umoja wa hiari unaowaunganisha watanzania wenye asili ya Iramba ama
kwa kabila, kuishi kusoma au kufanya kazi yoyote halali maeneo yanayozunguka
Iramba kama yalivyobainishwa kwenye historia fupi ya Iramba.
Madhumuni ya chama hiki ni kusaidiana katika masuala
mbalimbali ya kijamii na kiuchumi. Masuala ya kijamii ni pamoja na matatizo
mbalimbali yatakayomfika mwanachama kama vile magonjwa, misiba na majanga
mengineyo. Wanachama watashirikiana pia kwenye furaha, mafanikio na fursa
mbalimbali. Chama hiki pia kinalenga
kurahishisha maisha na kujenga mtandao wa kusukuma maendeleo ya Iramba katika
masuala ya huduma za kijamii na fursa mbalimbali za kiuchumi ndani na nje ya
Iramba kwa ujumla.
Kwa mantiki hiyo:
·
Chama kinaamini kwamba Iramba inazo
fursa nyingi za kijiografia, maliasili, rutuba, madini, mazao adimu, mazingira
na rasilimali watu ambazo kwa pamoja zikitumika vizuri zinatosha sana katika
kuongeza kipato kwa wana Iramba kwa ujumla wake
·
Chama kinaamini kwamba nguvu ya umoja wa
wana Iramba wote hapa nchini na nje bila kujali utofauti wa mitizamo vitaleta
mapinduzi na maendeleo na hatimaye kuitangaza vema Iramba na ijulikane zaidi
katika ramani ya ulimwengu huu.
Pia chama
kimeitikia wito wa serikali wa kuhamasisha wnachama wake kushiriki katika taasisi
za kiuchumi kama vile mpango wa akiba na
mikopo kupitia SACCOS ya chama na huduma za jamii kama vile Bima ya afya na
huduma zingine zitakazoanzishwa
Chama hiki hakitajihusisha na mambo ya kisiasa
na wala hautakumbatia sera na itikadi za kidini au chama chochote cha kisiasa.
Toleo
hili la katiba ya IDA litasomeka toleo na. 1 la mwaka 2016