1.
Kulipia
ada na michango yote halali ya chama
2.
Kuiheshimu,
kuilinda na kuitetea katiba ya chama na
kanuni zake
3.
kulinda
mali za chama
4.
Atalazimika
kuwa na kadi (kitambulisho) ya uanachama, katiba na kanuni zake
5.
Kuhudhuria
vikao vyote vinavyomhusu. Mwanachama
atakayechelewa kufika kwenye mkutano unaomhusu, atakayevuruga taratibu za
mkutano kwa makusudi na asiyehudhuria mikutano mitatu mfululizo bila kutoa
taarifa kwa katibu mkuu wa chama atachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa
mujibu wa kanuni za IDA
Atatakiwa kuwa mfano bora kwa
jamii, kuwa na nidhamu katika kauli na vitendo