- Baada ya kubuniwa
umoja huu iliundwa kamati teule iliyokuwa na wajumbe sita (6) kwa ajili ya
kuandaa nyaraka na rasimu ya katiba ya kuanzisha umoja ulitajwa katika
katiba hii
- Wajumbe wa kamati
teule walikuwa hawa wafuatao:
- Neema Kitainda Kitundu - Mwenyekiti
- Oscar Gyuzi Mkumbo - Mjumbe
- Emmanuel Metusela Msengi Urembo - Mjumbe
- Benadetha Mwanza - Mjumbe
- Noel Kyunsi - Mjumbe
- Albert Schinka Mazzuki - Katibu
- Kamati ya kuandaa
ajenda za mkutano mkuu wa uanzilishi kazi zake zitakoma baada ya uongozi
wa kipindi cha mpito kuchaguliwa
- Uongozi wa mpito
utachaguliwa na mkutano mkuu na utaendesha shughuli za IDA Makao makuu
katika kipindi chote cha mpito
- Muda wa uongozi wa
Mpito utakuwa miaka mitatu kuanzia tarehe ya kuanza kutumika Katiba hii
mara baada ya kuidhinishwa na Mkutano mkuu wa wanachama
- Mambo yafuatayo yatafanyika
na kukamilika ndani ya Muda wa
kipindi cha Mpito:
- Kuwezesha usajili wa
IDA kisheria
- Kutunga na
kurekebisha kanuni zote zitakazosimamia IDA makao makuu na matawi yake
- kuundwa kwa Taasisi
nyingine za kikatiba zilizoainishwa kwenye Katiba hii na kwa kuzingatia
masharti ya Katiba hii
- kufanya maandalizi
na mambo yote muhimu kwa ajili ya utekelezaji bora wa masharti ya kikatiba
yaliyomo kwenye Katiba hii
- kuwezesha
uanzishwaji wa mpango wa akiba na mikopo kwa ajili ya fursa za kiuchumi
kwa wanachama
- Kuwezesha uanzishwaji wa huduma ya bima ya afya kwa
wasio nazo
- Viongozi wa mpito
hawataguswa na masharti yeyote ya ukomo wa uongozi yaliyoinishwa katika
katiba hii